Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 07:56

Mkurugenzi wa IMF azuru Rwanda, akutana na mawaziri na magavana


IMF World Bank
IMF World Bank

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Fedha  IMF, Kristalina Georgieva yuko nchini Rwanda kwa ziara ya siku tatu.

Akiwa mjini Kigali amekutana na mawaziri wa fedha pamoja na magavana wa benki kuu za Rwanda, Uganda, Kenya na Sudan Kusini.

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kwamba shirika lake liko tayari kusaidia miradi mikubwa ya maendeleo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.

Amesema ili mataifa haya yaweze kufanikiwa kuna umuhimu wa kuandaa miradi mizuri ambayo inaweza kupata ufadhili hasa kwa kuzingatia kuwa pesa iliyopo haitoshi.

‘’ Hakuna pesa ya kutosha kwa shughuli za umma mahali popote kwa ajili ya miradi yanayohusu mabadiliko ya hali ya hewa, tunazungumzia mahitaji ya trilioni ya fedha zinazohitajika, lakini tunajadili pesa iliyopo ambayo ni mabilioni.

Labda tukitumia hizi billioni za fedha zilizopo kuandaa mazingira ya uwekezaji binafsi katika kiwango kinachotakiwa vinginevyo hatuwezi kufanikiwa, hatutafika popote.”

Aliongeza kusema kuwa: “Tunapokaa hapa kwenye ukumbi huu, ni kama tumegawanyika, na hili ndilo tatizo kwamba Benki ya Dunia wanafanya hili, Benki ya Maendeleo ya Afrika wanafanya lile, kila mmoja ana mradi wake, yote ni sawa tu lakini hayaendi popote.’’

Imetayarishwa na mwandishi wetu Sylivanus Karemera, Rwanda.

XS
SM
MD
LG