Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 16:46

Mkosoaji wa serikali ya Rwanda afariki dunia


Hayati mwandishi wa habari Ntwali John Williams wakati wa uhai wake.
Hayati mwandishi wa habari Ntwali John Williams wakati wa uhai wake.

John Williams Ntwali, mmoja wa waandishi wa habari wachache wa Rwanda waliochapisha habari zinazoikosoa serikali, amefariki dunia  gazeti lake la The Chronicles liliripoti.

Polisi waliambia gazeti la The Chronicles kwamba Williams alifariki katika ajali ya gari mapema Jumatano katika mji mkuu Kigali, gazeti hilo lilisema.

Hakuwapo kazini tangu Jumatatu, iliongeza.

Wanaharakati wa haki za binadamu na waandishi wa habari nje ya Rwanda mara moja waliuliza maswali kuhusu taarifa hiyo rasmi, wakibainisha jinsi wakosoaji wa serikali ya Rais Paul Kagame wamekuwa wakikamatwa mara kwa mara, kutishiwa, au kutoweka hapo awali.

Msemaji wa Polisi wa Rwanda John Bosco Kabera na msemaji wa serikali Yolande Makolo hawakujibu mara moja ombi la Reuters la kutaka maoni yao Ijumaa.

XS
SM
MD
LG