Nyaraka za mradi wa Benki ya Dunia zitaweka wazi kuwa LGBTQ wa Uganda hawabaguliwi na wafanyakazi hawatakamatwa kwa kuwajumuisha watu hao, Victoria Kwakwa, mkuu wa benki hiyo mashariki na kusini mwa Afrika, ameiambia Reuters.
Vikundi vya kutetea haki vimesema kuwa Sheria dhidi ya watu wenye mahusiano ya jinsia moja (AHA), zilizopitishwa mwezi Mei na kuweka adhabu ya kifo kwa baadhi ya mahusiano ya jinsia moja, imeibua wimbi la unyanyasaji dhidi ya watu wa LGBTQ, zaidi ikiwa watu binafsi.
“Tunafanya yote haya kuweka wazi hamtakiwi kuyafanya katika miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia na kusema unaruhusiwa kufanya hili kwa njia sahihi na hutakamatwa,” Kwakwa alisema, pembeni ya mkutano wa mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) huko Marrakech, Morroco.
Alisita kutoa muda wa kutathmini ufanisi wa hatua hizo na kuelekea kufanya maamuzi iwapo watarejesha tena ufadhili mpya kwa Uganda.
“Tumelijadili hili kwa urefu na serikali. Serikali inakubaliana na hilo,” kwakwa alisema.
Wakati Benki ya Dunia ilipositisha ufadhili mpya, maafisa wa Uganda waliishutumu taasisi hiyo ya maendeleo ya kifedha kwa unafiki, ikisema ilikuwa inakopesha kwa nchi za Mashariki ya Kati na Asia ambazo zina sheria kama hizo au kali zaidi zinazowalenga LGBTQ
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.
Forum