Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 08, 2024 Local time: 15:53

Kenya: Waislamu waandamana kupinga uamuzi wa Mahakama ya Juu kuhusu haki za LGBTQ


Waislam wakiandamana kupinga uamuzi wa mahakama, baada ya sala ya Ijumaa mjini Nairobi Oktoba 6, 2023. -AFP
Waislam wakiandamana kupinga uamuzi wa mahakama, baada ya sala ya Ijumaa mjini Nairobi Oktoba 6, 2023. -AFP

Mamia ya Waislamu katika mji mkuu wa Kenya leo Ijumaa  walikusanyika nje ya Mahakama ya Juu kupinga uamuzi wake wa mwezi uliopita wa kuthibitisha haki ya  jamii ya watu wenye uhusiano wa jinsia moja kujumuika.

Walisema kwamba hukumu hiyo inaunga mkono ukosefu wa maadili na kuwataka baadhi ya majaji wajiuzulu.

Maandamano hayo yamefanyika mjini Nairobi baada ya sala ya Ijumaa huku waandamanaji wakiwa wamebeba mabango yaliyoonyesha kwamba hukumu hiyo imefuata ukoloni mamboleo na kuwataka majaji watatu kati ya watano waliounga mkono uamuzi wa jopo la walio wengi, kutubu na kujiuzulu.

Baadhi ya wakristo wa- konsevativu walihudhuria pia.

Mwezi uliopita mahakama ilithibitisha uamuzi wa awali kwamba bodi ya mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Kenya yaliibagua jumuiya ya LGBTQ ilipokataa kusajili chama chao.

Majaji hao walitofautiana wakipinga uamuzi huo kwa misingi kwamba sheria za Kenya zinaharamisha uhusiano wa watu wa jinsia moja.

Jumuiya ya lgbtq nchini Kenya mara nyingi inalengwa na watu wanaochukia ushoga, ikiwa ni pamoja na visa vya manyanyaso ya kimwili na maneno .

Forum

XS
SM
MD
LG