Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 16, 2025 Local time: 18:37

Baraza la Seneti kupiga kura Jumatatu kumuidhinisha Jaji Barrett


Jaji Amy Coney Barrett
Jaji Amy Coney Barrett

Baraza la Seneti la Marekani baadaye Jumatatu linatarajiwa kupiga kura ya kumuidhinisha jaji mpya wa mahakama ya juu Amy Coney Barrett.

Iwapo Barrett ataidhinishwa, basi atakuwa jaji wa 3 kwenye mahakama hiyo yenye jumla ya majaji 9 kuteuliwa na Rais Donald Trump, swala ambalo huenda likabadili wingi wa majaji wa concervative kuwa 6 kwa watatu.

Maseneta wa chama cha Trump cha Repablikan ni 53 huku wale wa Demokratik wakiwa 47 ikiwa na maana kuwa wana uwezo wa kumuidhinisha jaji huyo bila shida.

Hata hivyo mmoja wao Susan Collins amesema kuwa hatoshiriki zoezi hilo kutokana na ushindani mkali ulioko kati ya wagombea urais kwenye uchaguzi mkuu utakao fanyika wiki ijayo.

Wajumbe wa Demokrat wamepinga kuidhinishwa kwa Barrett wakidai kuwa mchakato huo umefanywa kwa haraka zaidi wakati kukiwa na uchaguzi unaofanyika.

Wamedai kuwa jukumu la kujaza pengo lililoachwa baada ya kifo cha Jaji Ruth Bader Ginsburg lingesuburi hadi baada ya uchaguzi.

Kiongozi wa walio wengi kwenye seneta Mitch McConnel jana Jumapili amesifu hatua ya baraza hilo akisema kuwa mchakato wa kumteua Barrett utaendelea kama ilivyopangwa.

XS
SM
MD
LG