Balozi Thomas –Greenfield pia ametoa wito kwa Korea Kaskazini kuwa na majadiliano ya kweli na yenye tija na jirani yake, alipokua anatoa maelezo yake wakati wa ziara katika eneo la mpakani lisiloruhusiwa shughuli za jeshi –DMZ, kati ya hizo mbili za Korea ambazo kimsingi zimesalia katika hali ya vita.
Ziara ya balozi huyo huko Korea Kusini imekuja baada ya Russia kukataa urejeshaji upya wa kila mwaka wa jopo la wataalamu wa kimataifa ambalo kwa muda wa miaka 15 iliyopita lilifuatilia utekelezaji wa vikwazo vya Umoja wa Mataifa vinavyolinda kuzuiya mipango ya nyuklia na makombora ya Korea Kaskazini.
Moscow na Beijing zinatumia nyadhifa zao katika baraza la usalama kuilinda Korea Kaskazini katika uwajibikaji, Greenfield alisema, “na wacha niseme wazi, Marekani haina dhamira yoyote ya chuki dhidi ya DPRK, tuliomba mara kwa mara Pongyang kukataa uchochezi na kubaki na mazungumzo.”
“Tumeweka milango wazi kwa diplomasia yenye maana na tunabaki wazi kwa mazungumzo yenye tija bila masharti,” alisema.
Forum