Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 07:28

Seneti yathibitisha balozi Green kuongoza USAID


Balozi Mark Green alipokuwa Tanzania.
Balozi Mark Green alipokuwa Tanzania.

Baraza la Seneti la Marekani Alhamisi limethibitisha aliyekuwa Mbunge Mark Green ambaye ni chaguo la Rais Donald Trump kuongoza Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).

Balozi Green anachukuwa nafasi hiyo wakati ambapo uongozi wa Trump umependekeza kupunguza msaada wake na kuboresha shirika hilo.

Green alikuwa mwakilishi wa Chama cha Republikan cha Marekani kutoka Wisconsin kuanzia mwaka 1999 mpaka mwaka 2007, balozi wa Marekani nchini Tanzania chini ya utawala wa Rais mstaafu George W. Bush na rais wa Taasisi ya International Republican Institute, akijishughulisha na kutangaza demokrasia na utawala bora nje ya nchi.

Kipindi chake cha kutumikia USAID kinaanza katikati ya mpango wa uongozi wa Trump unaolenga kupunguza bajeti kwa asilimia 31ya taasisi hiyo na ya Wizara ya Mambo ya Nje.

Pia uteuzi wake umekuja wakati ambao mgogoro mkubwa wa wakimbizi unazikabili nchi za Ulaya na mwengine wa Mashariki ya Kati unaotokana na vita vinavyoendelea huko Syria na Iraq, balaa la njaa na ukame katika baadhi ya maeneo ya Afrika ambayo yamewaondoa maelfu ya wakazi kutoka katika maeneo yao.

Shirika hilo limetangaza Alhamisi raundi ya pili ya harambee kwa ajili ya kusaidia maeneo mengine zaidi yalioathiriwa na ukame katika nchi za Afrika.

Uteuzi wa Green umepokewa kwa shangwe kubwa na wataalamu wa maendeleo na makundi yanayotoa misaada.

XS
SM
MD
LG