Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 14:08

Burundi haijathibitisha ikiwa itahudhuria mazungumzo ya Arusha


Rais mstaafu Benjamini Mkapa
Rais mstaafu Benjamini Mkapa

Awamu nyingine ya mazungumzo ya kutafuta amani nchini Burundi yanatarajiwa kuanza Alhamisi mjini Arusha, Tanzania chini ya usimamizi wa rais mstaafu wa Tanzania Benjamini William Mkapa.

Kikao hicho kinachofanywa Alhamisi bado hakijapokea majina ya wajumbe wa serikali ya Burundi wataoiwakilisha katika mazungumzo hayo na hivyo kuzusha wasiwasi kuhusu kuhudhuria kwao.

Mazungumzo hayo yamelenga kufikia mkataba wa kumaliza mzozo wa kisiasa unaoikabili Burundi tangu rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza alipotangaza nia yake ya kugombea awamu ya tatu katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa serikali, chama tawala pamoja na upinzani wamesema kuwa wamesha pata mwaliko na baadhi wako tayari kushiriki katika kikao hicho mjini Arusha.

Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Allain Aime Nyamitwe amesema Nadhani ni mapema mno kujuwa wajumbe wa serikali katika mazungumzo hayo.

Hata hivyo kauli hiyo imezusha wasiwasi iwapo serikali ya Burundi itashiriki au la katika kikao hicho ambacho serikali wanasema hawawezi kukaa kwenye meza moja na wanasiasa wa upinzani ambao tayari wamealikwa na ofisi ya mpatanishi.

Hao ni wale walioondoka nchini ambao serikali inasema wanafuatiliwa na vyombo vya sheria vya Burundi.

Waziri amekariri msimamo wa serikali kwamba haiwezi kuzungumza na hao ambao imedai walishaamua kupambana kivita.

Lakini upande wa upinzani wamesema wako tayari kushiriki mazungumzo hayo.

Mjumbe wa chama cha upinzani cha Uprona, Evariste Ngayimpenda, tawi lisilokubaliwa na serikali anasema "tutakwenda, na tutatetea suala la kuheshimu mkataba wa Arusha na katiba iliyotokana na mkataba huo."

β€œNa ikiwa tutakubaliana tutapendekeza iundwe tume ya kufuatilia utekelezwaji wa mkataba huo.”

Hii ni awamu nyingine ya mazungumzo, Katika awamu ya kwanza mkataba wa amani ulitiwa saini mwaka 2000 na kuiwezesha Burundi kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyo dumu kwa muongo mmoja.

Washiriki katika mazungumzo haya wanapanga kuangalia kwa undani kipi kifanyike ili kumaliza mzozo wa kisiasa unaoikabili Burundi tangu Aprili mwaka wa 2015, alipotangazwa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kuwa atagombea urais katika awamu ya tatu.

Wajumbe zaidi ya 30 kutoka tabaka zote wamealikwa lakini hatua ya msimamizi wa mazungumzo haya ya kualika wanasiasa wanaofuatiliwa na vyombo vya sheria Burundi imeanza kulaaniwa na mashirika ya kiraia yaliokaribu na chama tawala.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Haidallah Hakizimana, Burundi

​
XS
SM
MD
LG