Uamuzi wa Faki wa Julai mwaka 2021 ulisababisha upinzani kutoka kwa wanachama wenye ushawishi ikiwemo Afrika Kusini na Algeria ambazo zilisema kwamba ilionyesha kubeza taarifa za AU kuunga mkono maeneo ya Palestina.
Macky Sall, Mwenyekiti wa AU na Rais wa Senegal anasema: "Tumejadiliana jambo hili kwa uwazi kabisa, kwa kweli lazima uone kwamba hilo ni jambo la kugawanya kwa sababu nchi zina misimamo tofauti. Na tulihisi kwamba Afrika haitakiwi kugawanywa na suala ambalo ni la kigeni”.
Nchi zote zilishinikiza suala hilo liwekwe katika agenda katika kipindi cha mjadala Jumamosi, Faki aliitetea uamuzi wake kwa Israel akigusia kwamba mataifa wanachama 44 wanaushirikiano wa kidiplomasia na Israel.
“tutaunda kamati ambayo lazima iwe chini ya uenyekiti wa Umoja wa Afrika , itafute masuluhisho, muafaka kama tunaweza kupata, yatapatikana, kama kamati hii haitaweza kupata makubaliano itapendekeza uamuzi au marekebisho ya uamuzi au itapendekeza kusitishwa kwa kuamuzi," aliongeza kusema Sall.
Facebook Forum