Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 19:26

Umoja wa Afrika(AU) wasitisha uwanachama wa Burkina Faso kufuatia mapinduzi ya kijeshi.


Kiongozi wa kijeshi nchini Burkina Faso, Paul Henri Sandaogo Damiba akizungumza kupitia televisheni ya taifa, Januari 27. Picha ya AFP.
Kiongozi wa kijeshi nchini Burkina Faso, Paul Henri Sandaogo Damiba akizungumza kupitia televisheni ya taifa, Januari 27. Picha ya AFP.

Umoja wa Africa AU umetangaza leo Jumatatu kwamba unasitisha uwanachama wa Burkina Faso kufuatia mapinduzi ya Januari 24 yaliyomuondoa madarakani Rais Roch Marc Kabore.

Baraza la Amani na Usalama la Umoja huo limeandika kwenye ujumbe wa Twitter kwamba wajumbe wake 15 wamepiga kura kusitisha Burkina Faso kushiriki kwenye shughuli zote za AU hadi pale utawala wa kikatiba unarudishwa nchini humo.

Jumuia ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS tayari ilishasitisha uwanachama wa Ougadougou tangu Ijuma na kupeleka ujumbe wakijeshi siku ya jumamosi kukutana na baraza tawala la kijeshi (MPSR).

Hii leo, Ujumbe wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za jumuia hiyo unatarajiwa katika mji mkuu wa Ougadougou, ambako utakuwa na mazungumzo pia na viongozi wa baraza hilo la kijeshi.

XS
SM
MD
LG