Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 09:18

Utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso watangaza hatua za kurejesha uongozi wa kikatiba


Kundi la wanajeshi likitangaza kumuondoa madarakani rais wa Burkina Faso. Picha ya Reuters, Januari 24, 2022
Kundi la wanajeshi likitangaza kumuondoa madarakani rais wa Burkina Faso. Picha ya Reuters, Januari 24, 2022

Utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso Jumatatu umetangaza kwamba umerejesha hali ya kutekeleza katiba ya nchi wiki moja baada ya kuchukuwa madaraka na kumteua kiongozi wa mapinduzi hayo kuwa mkuu wa nchi kwa kipindi cha mpito.

Hatua hiyo imejiri muda mfupi baada ya Umoja wa Afrika kusitisha uanachama wa Burkina Faso kutokana na mapinduzi ya kijeshi Jumatatu iliyopita, huku wanadiplomasia kutoka Afrika magharibi na Umoja wa Mataifa wakishinikiza kurejea kwa utawala wa kiraia.

Katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa, Baraza la utawala wa kijeshi MPSR limetangaza kuidhinisha “kitendo cha msingi” ambacho “kinaondoa kusitishwa kwa katiba”, hatua ambayo ilikuwa imetangazwa baada ya mapinduzi ya Januari 24.

Hati hiyo yenye vifungu 37 inahakikisha uhuru wa mahakama, kusheshimu uhuru wa mshukiwa hadi ibainike ana hatia, pamoja na uhuru wa kimsingi ulioelezwa katika katiba kama vile uhuru wa kutembea na uhuru wa kujieleza.

Taarifa hiyo haikutoa ratiba ya kipindi cha mpito.

Imemtambuwa rasmi kiongozi wa mapinduzi, Kanali Paul Henri Sandaogo Damiba kama rais wa Baraza la MPSR.

Amepewa pia majukumu ya rais wa Burkina Faso, na amri jeshi, taarifa hiyo imesema. Na kutakua na makamu rais wawili bila ya kutaja majina yao.

Katika amri tofauti ya utendaji iliyosomwa kwenye televisheni inasema kwamba mkuu wa utawala katika jeshi Gilbert Ouedraogo anaacha wadhifa wake.

Matokeo hayo yote yanafanyika wakati ujumbe wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa ECOWAS ukiongozwa na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ghana Shirley Ayorkor Botchway umewasili Ouagadougu na kuungana na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya nchi za Afrika Maghraibi Mahamat Saleh Annadif.

Ujumbe huo wa pamoja unatarajiwa kukutana na viongozi wa kijeshi na kuzungumzia mipango yao na kuwataka kurudisha utawala wa kiraia kwa haraka iwezekanavyo.

XS
SM
MD
LG