Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 07:19

Askofu Desmond Tutu atoka hospitali


Askofu Desmond Tutu
Askofu Desmond Tutu

Askofu Desmond Tutu, ambaye alishiriki katika kupambana na sera za ubaguzi na kuikomboa Afrika Kusini Ijumaa ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kupatiwa matibabu ya saratani ya tezidume.

Taasisi ya Desmond Tutu Foundation imetoa taarifa hiyo na kueleza kuwa Askofu Tutu ameruhusiwa kutoka hospitali na yuko nyumbani anapumzika ili kurejesha afya yake.

Tutu ambaye ametimiza miaka 87 alisherekea siku ya kuzaliwa kwake akiwa hospitalini.

Tutu alipata tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 1984 kutokana na harakati zake za kupiga vita ubaguzi wa rangi.

XS
SM
MD
LG