Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 15:12

Askari wa Tanzania aliyejeruhiwa DRC afariki


Miili ya askari wa JWTZ ilipokuwa ikiiagwa katika sherehe fupi ya kuwaenzi wapiganaji hao nchini Tanzania
Miili ya askari wa JWTZ ilipokuwa ikiiagwa katika sherehe fupi ya kuwaenzi wapiganaji hao nchini Tanzania

Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), aliyejeruhiwa katika shambulizi dhidi ya Walinda amani kutoka Tanzania, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mapema mwezi wa Dismeba amefariki akiwa anapatiwa matibabu Uganda.

Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa marehemu ni miongoni mwa wanajeshi waliokuwemo kwenye ngome ya walinda amani wa Jeshi la Umoja wa Mataifa linalojulikana kama (MONUSCO).

Ngome hiyo ilishambuliwa na waasi huko Semuliki, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kwa mujibu wa UN, askari waliofariki hadi sasa wamefikia 15. Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN, Stephane Dujarric, ametangaza kifo cha shujaa huyo katika mkutano na wanahabari huko New York, Marekani jana.

"Misheni ya UN huko DRC (MONUSCO) imethibitisha kuwa mlinda amani wa 15 amefariki huko Kampala...." taarifa ya UN imesema. Hata hivyo, UN imetuma salamu za rambirambi kwa ndugu wa marehemu, wananchi, serikali ya Tanzania na walinda amani wa umoja huo.

Katika taarifa yake Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa umeanza uchunguzi wa kina kuhusu shambulizi hilo na umeahidi kutoa taarifa haraka iwezekanavyo.

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani katika Umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix amesema uchunguzi unafanywa kwa kuzingatia vigezo vyote vya kimataifa.

Pia amesema baada ya kukamilika uchunguzi huo wataalamu watafanya uchambuzi na kutoa mapendekezo katika hatua ya kuzuia mashambulizi kama hayo kujirudia.

“Uchunguzi utafanyika kwa mbinu ambazo zinatakiwa. Hitimisho na mapendekezo yatachambuliwa kwa kina na kuzingatiwa kwa hali ya juu na kwa haraka iwezekanavyo,” amesema baada ya kutembelea kambi ya Semuliki iliyoko Kivu Kaskazini.

XS
SM
MD
LG