Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 05:33

APC yashinda Lagos


NIGERIA-POLITICS-VOTE

Chama tawala nchini Nigeria kimeshinda viti vingi vya katika uchaguzi wa magavana uliofanyika mwishoni mwa wiki, matokeo yameonyesha Jumanne, kufuatia upigaji kura uliogubikwa na ghasia, vitisho na ununuzi wa kura.

Uchaguzi wa magavana ulifanyika katika majimbo 28 kati ya 36, na pia uliwachagua wabunge wa majimbo. Magavana katika majimbo nane yaliyosalia walikuwa wamechaguliwa awali katika uchaguzi mdogo kutokana na maamuzi ya mahakama.

Uchaguzi wa serikali za mitaa umekuja wiki tatu, baada ya mgombea wa chama tawala cha All Progressives Congress (APC), Bola Tinubu, kushinda kura ya urais ambayo wapinzani walisema ilijaa wizi mkubwa.

Kwa mujibu wa matokeo ya kura ya Jumamosi iliyotangazwa na Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (INEC), APC ilishinda ugavana katika majimbo 15 -- Lagos, Sokoto, Katsina, Jigawa, Gombe, Kwara, Niger, Yobe, Nasarawa, Cross River, Ebonyi, Ogun, Benue, Kaduna na Borno.

Waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya wamesema Jumatatu takriban watu 21 waliuawa wakati wa uchaguzi huo wa kikanda nchini Nigeria, ambao ulikumbwa na vitisho, ghasia na idadi ndogo ya watu waliojitokeza kupiga kura.

Barry Andrews, Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa kutoka Umoja wa Ulaya (EU EOM) aliuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba Lagos, imemchagua tena gavana kutoka chama tawal. Lagos ni miongoni mwa majimbo kadhaa ya kusini na kati ambayo yalishuhudia ghasia zinazohusishwa na uchaguzi.

Upigaji kura siku ya uchaguzi, majimbo mengi yalishuhudia matukio mbali mbali ya ujambazi, manyanyaso kwa wapiga kura, wasimamizi wa uchaguzi, waangalizi na waandishi wa habari na hali hii ilitokea katika majimbo mengi ," Andrews alisema.

"Hii ni huzuni kubwa kwa watu 21 kupoteza maisha katika vurugu zinahusiana na uchaguzi, hii inatokana na taarifa zetu za hivi punde”.

Idadi ya vifo vilivyoripotiwa ilikuwa chini mno katika chaguzi za awali katika taifa hilo la Afrika lenye idadi kubwa ya watu barani humo.

Mwangalizi huyo alisema hata hivyo, kulikuwa na maboresho katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumamosi ikilinganishwa na uchaguzi wa rais uliozua mzozo mwezi uliopita. Vifaa vya uchaguzi viliwasili kwa wakati katika vituo vingi vya kupigia kura, ambavyo vilifunguliwa mapema huku mashine za elektroniki za kupiga kura zikifanya kazi vizuri zaidi kuliko mwezi uliopita.

Chanzo cha habari hii shirika la habari la Reuters na AFP

XS
SM
MD
LG