Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 30, 2022 Local time: 09:04

Angola: Upinzani wapinga matokeo ya uchaguzi katika mahakama ya katiba


FILE PHOTO: Angola opposition party UNITA holds final rally

Chama kikuu cha upinzani nchini Angola kimewasilisha kesi katika mahakama ya katiba ya taifa hilo, kupinga matokeo ya uchaguzi wa mwezi uliopita ambapo chama tawala cha People’s Movement for the Liberation of Angola (MPLA) kilitangazwa mshindi.

Uchaguzi wa Agosti 24 ulikuwa wenye ushindani mkali zaidi katika nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta tangu kura yake ya kwanza ya vyama vingi, mwaka 1992. Ikichukua zaidi ya asilimia 51 tu ya kura, tume ya uchaguzi ilitangaza MPLA kuwa mshindi - na kumpa Rais Joao Lourenco muhula wa pili.

UNITA - vuguvugu la zamani la waasi ambalo lilipigana vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 27 dhidi ya serikali ya MPLA vilivyomalizika mwaka 2002 - lilipata takriban asilimia 44 ya kura, matokeo yake bora zaidi, kwa mujibu wa tume ya uchaguzi.

Katika hotuba yake ya video, kiongozi wa UNITA Adalberto Costa Junior, mwenye umri wa miaka 60, alirudia kauli yake ya awali kwamba vuguvugu hilo "halitambui matokeo ya mwisho" kutoka kwa tume ya taifa ya uchaguzi.

Kiongozi huyo wa upinzani alisema alitarajia mahakama ya kikatiba na tume kufanya kazi zao kwa kulinganisha hesabu yao ya kura na hesabu ya kura ya chama, ambayo bado haijatolewa kikamilifu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG