Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 12:50

Angola kutuma majeshi DRC


Wanajeshi wa Kanda ya Afrika Mashariki (EACRF) wakilinda kambi ya Rumangabo iliyoko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Januari 6, 2023. Picha na Guerchom Ndebo/AFP.
Wanajeshi wa Kanda ya Afrika Mashariki (EACRF) wakilinda kambi ya Rumangabo iliyoko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Januari 6, 2023. Picha na Guerchom Ndebo/AFP.

Angola itatuma wanajeshi 500 katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili kulinda maeneo yanayoshikiliwa na waasi wa M23 baada ya bunge la nchi hiyo ya kusini mwa Afrika kuidhinisha Ijumaa upelekaji wanajeshi.

Ukosefu wa usalama umetawala katika maeneo tete ya mashariki mwa Congo kwa zaidi ya mwaka mmoja, kutokana na kuibuka tena kwa kundi waasi la M23, ambalo linadai kutetea maslahi ya Watutsi, ambapo wamekamata sehemu kubwa ya jimbo la Kivu Kaskazini nchini Congo.

Mgogoro huo umezua mzozo wa kidiplomasia kati ya Kongo na nchi jirani ya Rwanda, ambapo Kinshasa inaishtumu nchi hiyo kuwaunga mkono waasi, ikiwemo kutuma wanajeshi wake kwenye eneo la mashariki mwa Congo.

Rwanda inakanusha kuhusika na tuhuma hizo. Mwaka jana, Rais wa Angola Joao Lourenco alifanya mazungumzo ili kusuluhisha mgogoro huo, ambapo Rais wa Kongo Felix Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame walikubali kupunguza mivutano, lakini usitishaji vita uliotangazwa haukufanikiwa.

Wabunge wa Angola waliokuwepo katika kura iliyopigwa siku ya Ijumaa waliidhinisha kwa pamoja kutuma majeshi katika majimbo ya mashariki mwa Congo kwa kipindi cha mwaka mmoja

Waziri wa nchi wa Angola Francisco Furtado alisema mapema wiki hii kuwa upelekaji wa majeshi yake unaweza ukaigharimu nchi hiyo shilingi bilioni 11.2, lakini nchi hiyo inatarajia kupokea michango kutoka kwa mashirika ya kimataifa, ikiwa pamoja na Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.

Mwaka jana Kenya, Uganda na Burundi pia walituma majeshi yake eneo hilo la Mashariki mwa Congo kama sehemu ya jeshi la kikanda la Afrika Mashariki linalolenga kusaidia kumaliza ghasia za wanamgambo.

Chanzo cha habari ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG