Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 08:00

Angela Merkel Amepata Tena Ushindi Wa Kuiongoza Ujerumani


Chansela wa Ujerumani, Angela Merkel.
Chansela wa Ujerumani, Angela Merkel.

Angela Merkel ameshinda awamu ya nne ya uongozi kama chansela wa Ujerumani katika uchaguzi wa shirikisho ambao matokeo yake yalionekana hayaepukiki tangu kuanza kwa kampeni miezi mitatu iliyopita.

Lakini chama chake tawala cha Christian Democrat kilipata kura chache kuliko ilivyotabiriwa na chama maarufu cha mrengo wa kulia nchini Ujerumani kilipata kura nyingi kuliko wakusanyaji maoni walivyobashiri.

Kwa kawaida matarajio yanalinganishwa na ukusanyaji maoni uliotolewa muda mfupi baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa na hivyo kukipa chama cha Merkel cha Christian Democratic Union na chama shirika Bavaria cha Christian Social Union kupata asilimia 32.5 ya kura na kumuweka katika mwelekeo wa kuwa mmoja wa chansela kati ya watatu kuchaguliwa kuongoza awamu ya nne baada ya vita.

Ukusanyaji maoni ulibashiri kuwa CDU na CSU wangepata ushindi wa asilimia 36 mpaka 39 ya kura.

XS
SM
MD
LG