Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 16, 2025 Local time: 18:55

Aliyetoroka jela kwa helikopta afunguliwa mashitaka Ufaransa


Franck Berton, wakili wa Faid Redouane (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika mahakama ya Saint-Omer, Februari 27, 2020. Picha na FRANCOIS LO PRESTI / AFP.
Franck Berton, wakili wa Faid Redouane (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika mahakama ya Saint-Omer, Februari 27, 2020. Picha na FRANCOIS LO PRESTI / AFP.

Mfungwa aliyeishangaza Ufaransa, ambaye alitoroka gerezani mwaka 2018 akiwa kwenye helikopta iliyotekwa nyara amefunguliwa mashitaka Jumanne mjini Paris, huenda akakabiliwa na kifungo cha maisha jela kwa utoro kwake.

Mtuhumiwa huyo ni Redouine Faid mwenye umri wa miaka 51, ambaye jina lake la utani ni "mfalme mtoro", alikuwa akitumikia kifungo baada ya kukutwa na hatia ya wizi wakati wenzake walipoiteka nyara helikopta na kutua katika uwanja wa gereza la Reau, lililopo kusini mashariki mwa Paris, asubuhi ya Julai mosi, 2018.

Wakati mmoja wao akiwa amemuwekea rubani bunduki kichwani, wengine wawili walitoka kwenye helikopta hiyo na kurusha magruneti ya moshi.

Mmoja wao kisha aliendelea kutoa uangalizi, akiwa na bunduki aina ya Kalashnikov, huku mwingine -- akiwa amevaa alama bandia za polisi mkononi -- alitumia msumeno wa umeme kulikata lango linaloelekea baraza la gereza alikofungwa Faid na kaka yake Brahim.

Walioshuhudia baadaye walisema kuwa Faid "kwa utulivu mkubwa" alitoka nje ya chumba chake na kwenda kwenye helikopta iliyokuwa ikimsubiri, ambapo ilipaa bila kufyatuliwa risasi. Operesheni nzima ilichukua dakika kumi. Polisi baadaye waliipata helikopta hiyo ikiwa imetelekezwa.

Miezi mitatu baadaye alikamatwa tena, akiwa amejificha katika nyumba ya rafiki wa jamaa yake.

Faid alitoka jela hapo awali mwaka 2013, alipowachukua walinzi na kulipua lango la gereza, anakabiliwa na kifungo cha maisha kwa kurudia kosa hilo.

Ana historia ya ujambazi unaohusisha kuiba magari ya kivita na kuwachukua watu mateka na wakati alipotoroka jela alikuwa tayari anatumikia kifungo cha miaka 25 kwa kosa la wizi ambalo lilisababisha mauaji ya polisi mmoja mwanamke.

Washukiwa kumi na mmoja wakiwemo Faid na wanafamilia yake wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kumsaidia kutoroka. Imechukua miezi mitatu mfululizo polisi kuweza kumkamata.

Chanzo cha habari ni Shirika la habari AFP

Forum

XS
SM
MD
LG