Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 04:16

Ajali Kenya zaua watu 9 na kujeruhi 21


Ramani ya Kenya
Ramani ya Kenya

Watu tisa wamepoteza maisha na zaidi ya 21 kujeruhiwa katika ajali mbalimbali za barabarani katika kipindi kisichozidi masaa ishirini na nne.

Ajali zote hizo zimetokea katika kaunti za Murang’a na Kisumu.

Huko Makuyu, watu watano walipoteza maisha na wengine tisa kujeruhiwa vibaya sana wakati gari yao waliokuwa wakisafiria kugongana na lori katika eneo la Mlima Swara blaclspot, karibu na shamba la Kakuzi, kwenye barabara kuu ya Nairobi-Nyeri.

Mkuu wa polisi wa Makuyu Paul Wanjama amesema lori hilo lilikuwa mali ya Kampuni ya Kakuzi limited lililokuwa likisafirisha mbao liliacha njia baada ya dereva kushindwa kulidhibiti na kugonga magari mawili siku ya Alhamisi usiku.

Katika ajali hiyo wanawake wanne na mwanamume moja waliuawa hapo hapo, amesema.

Majeruhi wa ajali hiyo pia walipelekwa hospitali ya Thika Level 5.

Wanjama amesema magari mawili ya matatus, moja linalo milikiwa na kampuni ya Ketno Sacco na jengine la Emuki Sacco, yalikuwa yakielekea Embu kutokea Nairobi ajali hiyo ilipotokea.

Mabaki ya magari ya matatus yaliyoharibika yalivutwa mpaka kituo cha polisi cha Makuyu.

Eneo la Ahero, watu wanne wameuawa na wengine 12 kujeruhiwa wakati gari ya matatu ilipogongana kwenye Barabara ya Ahero-Katito Ijumaa asubuhi.

Walofariki katika ajali hiyo walikuwa watu kutoka katika familia moja.

Walikuwa wako njiani kwenda Bondo kuhudhuria mahafali ya kuhitimu masomo ya mtoto wao wa kike katika Chuo Kikuu cha Jaramogi Oginga Odinga.

XS
SM
MD
LG