Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 27, 2023 Local time: 05:27

Ajali ya Nakuru yaua watu 19


Ramani ya Kenya.

Watu 19 wamepoteza maisha na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya basi kugongana uso kwa uso na lori nchini Kenya.

Ajali hiyo imetokea eneo la Mbaruk Jumamosi katika barabara kuu ya Nakuru-Nairobi, Mkuu wa polisi Nakuru, Hassan Barua amesema.

Kwa mujibu wa gazet la Daila Nation, basi hilo ambalo ni mali ya kampuni ya Highway Sacco lilikuwa linaelekea Busia likitokea Nairobi wakati ajali hiyo inatokea.

Kamanda Barua amesema dereva wa basi hilo alikuwa anajaribu kulipita lori ndipo alipogonga gari la mzigo lilokuwa linakuja mbele yake.

Dereva huyo alikimbia baada ya kutokea ajali hiyo, wamesema polisi.

Watu kumi na nne wamelazwa hospitali ya St Mary Nakuru, Shadrack Musau ambaye ni muuguzi wa zamu amesema.

Jumamosi jioni, rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alituma risala za rambi rambi kwa familia za waliopoteza maisha yao kwenye ajali hiyo na kuwafariji waliojeruhiwa.

"Nimehuzunishwa mno na habari kuhusu vifo vya watu 19 kwenye ajali hiyo iliyotokea Roysambu, Nakuru," Uhuru alisema kupitia taarifa ya ikulu.

Kenyatta aliamuru polisi na taasisi zingine husika kufanya uchunguzi wa kina kubbaini chanzo halisi cha ajali hiyo.

Ajali hiyo imeijiri taakriban wiki moja baada ya nyingine iliyowaua watu 35 katika nchi jirani ya Tanzania, wengi wao wakiwa wanafunzi wa shule.

XS
SM
MD
LG