Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 22:25

Ajali ya basi yaua watu 27 Kenya


Ramani ya Kenya
Ramani ya Kenya

Polisi Kenya wamesema watu 27 wamepoteza maisha baada ya basi na lori lenye trela kugongana.

Polisi wamesema kuwa ajali hiyo imetokea kwenye barabara kuu inayounganisha miji mikubwa miwili, ambayo ni makao makuu, Nairobi na mji wenye bandari, Mombasa.

Leornard Kimaiyo, mkuu wa polisi katika eneo la Kambu lilioko kaunti ya Maukeni, amesema basi lilikuwa linaelekea Mombasa na trela ilikuwa inapishana nalo kwenda upande mwengine zilipogongana Jumanne.

Ajali za barabarani zinasababisha vifo vya watu takriban 3,000 Kenya kila mwaka.

Vifo vinavyotokana na ajali za barabarani vimeongezeka katika miaka ya karibuni juu ya kwamba kumekuwa na udhibiti wa walevi wanaoendesha magari.

Pia serikali imeweka faini kubwa na pia vifaa vya kubaini mtu amelewa katika vizuizi katika barabara mbalimbali.

XS
SM
MD
LG