Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 18:27

Ajali ya barabarani yaua watu 5 Kenya


Watu watano wamepoteza maisha Jumamosi usiku katika ajali ya kutisha ya barabarani karibu na makutano ya barabara kuu ya Nakuru-Eldoret.

Afisa usalama wa Barabarani Rift Valley Zero Arome amethibitisha ajali hiyo iliyotokea saa tatu usiku, iliyohusisha gari ya kusafirisha abiria (matatu) iliyokuwa inaelekea Eldoret baada ya kugongana na malori mawili.

Tukio hilo la ajali limetokea katika eneo la Kware karibu na njia panda ya Makutano kwenye kona kali sana ambayo inapita katika pori zito la Koibatek.

Sehemu hiyo ni kiasi cha kilomita 15 kutoka mahali ambapo wanamuziki sita wa Kalenjin na dereva waliuawawa katika daraja la Kamara na ni kilomita 20 kutoka eneo la Sachangwan, ambalo ni eneo hatari kwa ajali ambapo pia watu kadhaa hivi karibuni waliangamia katika ajali tofauti iliyohusisha magari zaidi ya 13.

Barabara hii mpaka sasa imeuwa zaidi ya watu 40 katika kipindi kisichopungua wiki moja.

Mpaka sasa Arome amesema bado wanasubiri maelezo zaidi kuhusu kilichosababisha ajali hiyo-- ili kujua ni watu wangapi wamekufa.

Kwa mujibu wa afisa huyo miili ya wale walikufa katika ajali hiyo imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti huko Eldama Ravine ikisubiri kutabuliwa na ndugu za marehemu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG