Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Leonce Rwegasira amesema ajali hiyo ilitokea asubuhi Jumatatu.
Alitaja magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni basi la Kampuni ya AJ Safari lenye namba za usajili T 497 BJB lililokuwa likitoka Lushoto kwenda Dar es Salaam na Hiace ikitoka Mkata kwenda Segera yenye namba T591 AKE.
Aliwataja waliokufa kuwa ni pamoja na dereva wa Hiace aliyefahamika kwa jina moja la Shabaan, wengine majina yao hayajatambulika na maiti zao zimehifadhiwa Kwenye Hospitali ya Magunga wilayani Korogwe.
ACP Rwegasira alisema majeruhi ambao hawakuchukuliwa majina yao ni kutokana na uharaka wa kuwasaidia kuwafikisha katika Kituo cha Afya Kabuku kwa ajili ya kuendelea na matibabu.