Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 22:59

Afrika yalegea katika utoaji wa chanjo za Covid-19


Mwanamke apokea chanjo ya Covid mjini Soweto Afrika kusini
Mwanamke apokea chanjo ya Covid mjini Soweto Afrika kusini

Shirika la afya duniani WHO Jumanne limesema kwamba huenda Afrika isifikie lengo lake la kutoa chanjo kwa asilimia 70 ya watu wake bilioni 1.3 dhidi ya COVID kufikia nusu ya pili ya 2024, lengo ambalo tayari mataifa mengi tajiri yamefikia. 

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, onyo hilo limetolewa wakati ulimwengu ukikabiliana na aina mpya ya virusi vya omicron. Baadhi ya mataifa tajiri yameidhinisha dozi ya tatu ya booster kwa watu wake, wakati chini ya asilimia 8 ya watu wa Afrika wakiwa wamepokea chanjo kamili.

Flavia Senkubuge ambaye ni mkuu wa chuo cha dawa cha Afrika kusini wakati akizungumza na wanahabari kwenye kikao cha WHO, amesema kwamba tatizo hilo haliwezi kumalizika kama ulimwengu hautashirikiana pamoja.

Ni mataifa 20 pekee kati ya 54 barani Afrika ambayo yametoa chanjo kamili kwa takriban asilimia 10 ya watu wake wakati mataifa 10 pekee yakiwa yametoa chanjo chini asilimia 2 kwa watu wake barani humo. Kufikia sasa Afrika imepokea takriban dozi milioni 434 wakati 910,000 zikisemekana kuharibika kwenye mataifa 20.

XS
SM
MD
LG