Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 15:05

Afrika Mashariki iko katika shauku kujua uamuzi wa kesi ya kupinga matokeo Kenya


Mgombea Raila Odinga na wafuasi wake wakiwasilisha nyaraka za kupinga matokeo ya uchaguzi Mahakama ya Juu mjini Nairobi, Kenya, 22 August 2022.
Mgombea Raila Odinga na wafuasi wake wakiwasilisha nyaraka za kupinga matokeo ya uchaguzi Mahakama ya Juu mjini Nairobi, Kenya, 22 August 2022.

Mahakama ya Juu inatarajiwa kutoa uamuzi juu ya masuala tisa yaliyowasilishwa na  wapinzani wanaopinga matokeo ya uchaguzi yakijikita katika maadili ya uchaguzi na uhalali wa kumtangaza naibu Rais William Ruto kuwa rais mteule.

Ni wakati mgumu kwa Kenya wakati nchi inasubiri uamuzi wa Mahakama ya Juu kwa kesi inayopinga matokeo ya uchaguzi wa rais iliyofunguliwa na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga na wengine.

Mahakama ya Juu inatarajiwa kutoa uamuzi Septemba 5 juu ya masuala tisa yaliyowasilishwa na wanaopinga matokeo hayo kuhusu maadili ya uchaguzi na uhalali wa kutangazwa Naibu Rais William Ruto kuwa rais mteule.

Mjadala huo umekuwa ukilenga uwezekano wa maamuzi mbali mbali katika kesi hiyo, huku wataalam wa kisheria wakitabiri mambo matatu.

Mahakama inaweza kukubaliana na uamuzi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) katika kumtangaza William Ruto ndiye rais mteule, au inaweza kubatilisha uchaguzi na kuamuru uchaguzi mpya.

Pia kuna wachache wanaofikiria huenda mlalamikaji anaweza kupewa ushindi.

Majaji saba walijitenga Ijumaa kwenda kufanya uamuzi wao wa kisiasa baada ya kukamilisha kusikiliza hoja za wanaopinga matokeo.

Bw Odinga, kiongozi wa upinzani ambaye ameshindwa uchaguzi wa urais kwa mara ya tano kwa kura chache, anadai kwamba kulikuwa na wizi katika uchaguzi na ameitaka Mahakama ya Juu ama ibatilishe matokeo yaliyotangazwa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Agosti 15 na iamuru uchaguzi urudiwe au atangazwe yeye ndiyo mshindi.

His legal team argued in court that there was massive vote rigging, citing certain discrepancies in vote count entries at polling stations and those transmitted electronically to the national tallying centre in Nairobi.

Timu yake ya wanasheria ilidai mahakamani kwamba kulikuwa na wizi mkubwa wa kura, ikieleza baadhi ya dosari katika kusajili hesabu ya kura katika vituo vya kupiga kura na zile zilizotumwa kielektroniki kwenye kituo cha taifa cha majumuisho ya kura mjini Nairobi.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la "The East African" linalochapishwa Kenya

XS
SM
MD
LG