Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 06:29

Afrika Kusini yaripoti kushuka kidogo kwa idadi ya vifaru wanaouliwa na majangili


FILE - Vifaru wkaiwa katika hifadhi ya wanyama ya Hluhluwe-Imfolozi nchini South Africa, Dec. 20, 2015.
FILE - Vifaru wkaiwa katika hifadhi ya wanyama ya Hluhluwe-Imfolozi nchini South Africa, Dec. 20, 2015.

Idadi ya vifaru wanaouliwa kwa ajili ya pembe zao nchini Afrika Kusini imepungua kidogo mwaka 2022, lakini hatua  zaidi lazima zichukuliwe  ili kuwaokoa vifaru hao katika mbuga zilizoko kwenye majimbo, wizara ya mazingira ilisema Jumatatu.

Jumla ya vifaru 448 kutoka maeneo mbalimbali nchini humo waliuwawa kinyume cha sheria mwaka jana 2022, mara tatu chini ya idadi ya waliouwawa mwaka 2021. Hata hivyo, takwimu bado zinaonyesha idadi kubwa kuliko zile za mwaka mmoja kabla, wakati masharti ya kudhibiti COVID-19 nchini Afrika Kusini yalisababisha kupungua kwa ujangili.

Mahitaji ya pembe za faru yamepunguza idadi ya wanyama hao kwa miongo mingi Afrika Kusini na nchi nyingine jirani za Botswana na Namibia. Mara nyingi ujangili unahusisha ushirikiano wa uhalifu wa kimataifa na wawindaji haramu wa maeneo hayo, ambayo husafirisha kwa magendo pembe hizo kimataifa.

Pembe hizo zinatumika kama dawa na vito vya mapambo katika baadhi ya nchi za Asia Mashariki.

Ujangili wa vifaru umepungua katika mbuga za wanyama za taifa za Afrika Kusini kutokana na progamu za kuondoa pembe za vifaru, kuimarisha ulinzi na ushirikiano kati ya mamlaka za mazingira na hifadhi, waziri wa Mazingira Barbara Creecy alisema.

Hata hivyo, alitoa wito kwa mamlaka za jimbo kufanya mengi zaidi, akisema wawindaji haramu sasa wamehamisha mwelekeo wao kutoka mbuga za kitaifa kwenda mbuga za mkoa na hifadhi binafsi katika jimbo la KwaZulu-Natal.

Afrika Kusini ni nchi yenye idadi kubwa sana ya vifaru weupe wanaotishiwa maisha na takribani nusu vifaru weusi wako hatarini barani Afrika .

XS
SM
MD
LG