Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 15:25

Afrika Kusini yampongeza DJ Black Coffee kwa tuzo ya Grammy


DJ Black Coffee akiwa nje ya club Altitude Beach, Fourways Johannesburg, March 21 2021. Picha: AFP
DJ Black Coffee akiwa nje ya club Altitude Beach, Fourways Johannesburg, March 21 2021. Picha: AFP

Afrika kusini imempongeza DJ Black Cofee baada ya kushinda tuzo ya kwanza ya Grammy, Jumapili.

Alishinda tuzo ya dansi na muziki bora kabisa kutokana na album yake ambayo imewavutia watu wengi.

Black Coffee alisema tuzo yake ni kwa heshima ya waafrika wanaochipukia na kukuza vipaji vyao.

Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa amemshukuru kwa kuwapa motisha kizazi kipya.

Mwimbaji Angélique Kidjo alishinda tuzo ya muziki bora wa mwaka kutokana na album yake inayohusu mazingira, ambayo aliwashirikisha wanamuziki wa Nigeria Burna Boy, Yemi Alade na Mr Eazi.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 61, aliwashinda Wizkid, Femi Kuti wa Nigeria, na Rocky Dawuni wa Ghana kwa tuzo hiyo, ambayo ni yake ya tano ya Grammy.

XS
SM
MD
LG