Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:34

Afrika Kusini yawika katika mbio fupi


 Kijana Tshenolo Lemao akimaliza fainali ya mita 100m kwa wavulana mjini Nairobi, Pembeni ni mshiriki Dos Santos kutoka Brazil.
Kijana Tshenolo Lemao akimaliza fainali ya mita 100m kwa wavulana mjini Nairobi, Pembeni ni mshiriki Dos Santos kutoka Brazil.

Vijana wa Afrika Kusini walichukua nafasi hiyo na “kung’ara” katika mbio za mita 100 kwa wavulana – wakishinda medali ya dhahabu na fedha katika shindano la fainali.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa Tshenolo Lemao alishindia Afrika Kusini dhahabu ya kwanza ambayo pia ni medali ya kwanza kutwaliwa katika amshindano hayo ya dunia mwaka huu, akiweka muda bora zaidi wa sekunde 10:57.

Aliyefuata katika nafasi ya pili pia ni kijana kutoka Afrika Kusini Retshidisitwe Lemao kwa muda wa sekunde 10:61 na kuipa Afrika Kusini medali ya pili, kisha nafasi ya tatu alikuwa ni Tyreke Wilson kutoka Jamaica ambaye aliwasili Nairobi akiwa na muda wa kasi zaidi mwaka huu kwa vijana chipukizi duniani.

Katika siku ya kwanza pia iliandaliwa fainali ya mbio za mita elfu 3,000 (tambarare) kwa wasichana ambapo Abersh Minsewo kutoka Ethiopia aliibuka bingwa mpya wa dunia, mbele ya mwenyeji Emmaculate Chepkurui aliyeshangiliwa na Wakenya wennzake uwanjani Kasarani.

Chepkurui sasa ameshindia Kenya medali ya kwanza ambayo ni fedha kwa muda wa dakika 9:24:69 mbele ya mpinzani mwingine kutoka Ethiopia Yitayish Mekonene aliyetwaa nishani ya shaba kwa muda wa dakika 9:28:46.

Kufikia Jumatano usiku wakati ratiba ya siku ya kwanza ilipokamilika Afrika Kusini ilikuwa ikiongoza mataifa yote zaidi ya 120 yanayoshiriki mashindano hayo, ikiwa tayari imepata medali mbili – dhahabu moja na fedha moja.

Ethiopia ilishikilia nafasi ya pili kwa kuzoa dhhabu moja pia sawa na Ujerumani iliyoshikilia nafasi ya nne. China ilikuwa katika nafasi ya 4 ikiwa na fedha moja sawa na wenyeji Kenya walioshikilia nafasi ya tano ikiwa mbele ya Jamaica.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliambatana na rais wa shirikisho la kimataifa la riadha (IAAF) Sebastian Coe kuyafungua rasmi mashindano hayo ya ubingwa wa chipukizi duniani, katika uwanja wa kimataifa wa Moi-Kasarani jijini Nairobi.

Rais Kenyatta alitangaza kuwa raia watayatazama mashindano hayo ya siku tano bila kulipa pesa yoyote ya kuingia uwanjani.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Josephat Kioko, Kenya

XS
SM
MD
LG