Okeyo, ambaye ni Katibu Mkuu na Makamu wa Rais wa Riadha wa zamani Kenya na pia ni mjumbe wa Baraza la Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF), na Joseph Kinyua, Mweka Hazina wa zamani wa riadha Kenya, walikuwa wanachunguzwa na bodi ya maadili ya michezo kuhusiana na malipo yaliyo fanywa na kampuni ya Nike ya Marekani inayo tengeneza nguo za michezo kwa kipindi cha miaka tisa.
Katika hukumu iliyo tolewa Alhamisi, bodi hiyo imegundua Okeyo alikuwa hajaweka wazi malipo mengi yaliyo fanyika kwa shirikisho la riadha Kenya, na kukiuka maadili katika matukio 10 baada ya kuchukua fedha za ufadhili ambazo zingeweza kutumika kwa njia bora zaidi kusaidia maendeleo ya michezo ya wana riadha Kenya na hivyo kufukuzwa kutoka katika nafasi yake kwenye Baraza la IAAF.
Kinyua amegundulika na bodi hiyo kujihusisha na vitendo kama hivyo lakini kwa kuwa nafasi yake ilikuwa haiwajibishwi na sheria za maadili zilizopo wakati huo alinusurika kuwekewa vikwazo.
Maafisa wote wawili wamekanusha kufanya makosa, wakisema kuwa malipo ya pesa hizo yalikuwa halali kwa matumizi yao wenyewe na ujuzi waliokuwa wakitoa.
Kinyua ameiambia Reuters Alhamisi kuwa alikuwa ameridhishwa na uamuzi huo na haki ilikuwa imefanyika.