Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 05:23

Afghanistan yakabiliwa na uhaba mkubwa sana wa chakula


Wapiganaji wa Taliban wakisherehekea mwaka mmoa tangu kuchukua mji mkuu wa Afghanistan Kabul, mbele ya Ubalozi wa Marekani Kabul Afghanistan, Jumatatu Aug. 15, 2022.
Wapiganaji wa Taliban wakisherehekea mwaka mmoa tangu kuchukua mji mkuu wa Afghanistan Kabul, mbele ya Ubalozi wa Marekani Kabul Afghanistan, Jumatatu Aug. 15, 2022.

Tangu kuondolewa maelfu ya washirika raia wa Afghanistan kufuatia kujiondoa kwa Marekani nchini humo mwaka mmoja uliopita, Wizara ya Mambo ya Nje imekuwa na jukumu la kuangalia jinsi ya kuwapatia misaada ya kibinadamu raia hao wanaishi chini ya Taliban huku kukiwa na uhaba mkubwa sana wa chakula.  

Makundi ya haki za binadamu na mashirika ya misaada yanasema hali kwa watu wa Afghanistan ni janga, huku baadhi wakiuza viungo vyao vya ndani ya mwili au watoto wao ili waweze kuishi. Mwaka mmoja baada ya wanajeshi wa Marekani na wanadiplomasia kuondoka, Marekani bado ni mfadhili mmoja mkuu wa misaada ya kibinadamu nchini humo. Fereshta Abbasi ni mtafiti wa Afghanistan katika Human Rights Watch.

Fereshta Abbasi, wa shirika la haki za binadamu (HRW) anaeleza: “Kwa mujibu wa takwimu za karibuni ni kwamba Shirika la Mpango wa Chakula limechapisha, kuwa asilimia 90 ya raia wa Afghanistan wanakabiliwa ya ukosefu wa chakula mwaka mmoja baada ya Taliban kuchukua majukumu. Watu wanakufa njaa. Ina maana kwambawatu hawana chakula.”

Taliban ilisherehekea wakati wakiadhimisha mwaka mmoja Jumatatu tangu kuchukua tena madaraka kutoka kwa serikali iliyokuwa ikiungwa mkono na Marekani mjini Kabul, wakisema wanatafuta uungaji mkono wenye nguvu wa kisiasa na uhusiano wa kiuchumi na nchi zote katika eneo hilo na dunia.

Lakini utawala wa Biden unahoji uhakikisho wa Taliban.

Akielezea mauaji ya mwezi uliopita ya kiongozi wa al-Qaida Ayman al-Zawahiri katika shambulizi la drone akiwa kwenye nyumbani kwake katikati ya Kabul, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Ned Price alisema kuwa utawala wa Biden hauko tayari katika misingi ya kuachilia fedha ambazo zinashikiliwa na Marekani kwa ajili ya Benki Kuu ya Afghanistan, lakini imekuwa katika mashauriano ya benki kwa miezi kadhaa kujaribu kutafuta suluhisho.

Price ameongeza kusema:“Hivi sasa, tunaangalia nyenzo ambazo zinazoweza kuwekwa ili kuona kuwa hizi dola bilioni tatu na nusukama akiba iliyohifadhiwa ili kutumiwa kwa ufanisi kwa ajili ya watu wa Afghanistan kwa njia ambayo fedha hizo hazi badili mwelekeo na kwenda kwa makundi ya kiaidi au kwingineko.”

Watalaam wameiambia VOA kwamba kiongozi wa al-Qaida alikuwa akiishi katikati ya Kabul na familia yake na imekuwa pigo kubwa kwa juhudi za kutaka kuachiliwa fedha na mali hizo.

Naye Michael Kugelman, wa Kituo cha Wilson Center amesema: “Hivi sasa nadhani kutokana na kile ambacho kimetokea kwa al-Zawahiri Marekani huenda ikachukua msimamo mkali sana na hawatakubali aina yoyote ya mipango ya kuziachia hizo fedha kwenda kwenye udhibiti wa Afghanistan mpaka kuwepo na njia ya wazi kabisa, aina fulani ya mfuko ambao utakuwa unasimamia hizo fedha mbali na Taliba ambayo inaweza kujaribu kufanya chochote. Taliban nayo itachukua msimamo mkali. Taliba, kwa sababu za kisiasa, lazima ihakikishe uhalali wa watu wake katika kufanya kazi.”

Watalaamu akiwemo Abbasi wanasema jumuiya ya kimataifa, ikiwemo Marekani, kwa hakika wanahitaji kuongeza misaada ya kibinadamu kwa raia wa Afghansitan. Lakini pia wanaitaka Taliban kufikiria vipaumbele vyao na kushughulikia mahitaji ya msingi ya watu badala ya kuweka masharti kwa haki za wanawake nchini Afghanistan.

XS
SM
MD
LG