Abiria wote walifanyiwa uchunguzi maalum wa kiafya na baadaye kuruhusiwa kuingia nchini humo.
Wakati huohuo Wizara ya Afya imesema abiria walishauriwa kujitenga kwa muda wa siku 14 kama hatua ya tahadhari dhidi ya uwezekano wa kusambaza virusi vya corona.
Hii ni mara ya kwanza kwa idadi kubwa ya abiria kuambiwa kujitenga na watu wengine.
Waziri wa Afya, Sicily Kariuki amesema katika taarifa yake kwamba kesi 17 za washukiwa wa virusi vya corona zimeripotiwa nchini humo, lakini wote waliofanyiwa uchunguzi wa kiafya wamegundulika hawajaambukizwa virusi hivyo.
Hata hivyo amewaasa raia wa Kenya kutofanya safari ambazo si muhimu kwenda kwenye nchi ambazo zimethibitishwa kuwa zina kesi za virusi vya corona.
Wakenya wengi wamestushwa na uamuzi wa serikali kuruhusu abiria kutoka China kuingia nchini.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.