Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 02:25

Burundi mvutano ndani ya chama cha FNL


Wakati msuko suko wa kisiasa unaendelea huko Burundi, chama kingine cha kisiasa cha kabiliwa na mvutano kati ya viongozi wake wa juu.

Chama cha zamani cha waasi FNL kimekumbwa na mzozo wa ndani baada ya kiongozi wake Agathon Rwassa kutangaza kwamba anamfukuza msemaji wake na msemaji wa chama Pasteur Habimana.

Hatua hiyo yake imewasababisha wanachama wake kugawika kukiwa na baadhi wanaomunga mkono Habiamana na wanaomunga mkono Bw Rwassa. Siku ya jumanne kiasi ya wajumbe 500 wanaomunga mkono msemaji wa chama walokutana mjini Bujumbura siku na miongoni mwa mambo mengine walitangaza kwamba hawautambui uwongozi wa Bw Rwassa.

Lakini akizungumza na sauti ya Amerika Bw. Habimana, anasema anamini yeye binafsi hajafanya kosa lolote na kwamba ilibidi kiongozi wa chama kufikisha malalamiko yake mbele ya kamati maalum ya chama kutanzua matatizo yao. Anasema yeye yungali anamtambua Bw Rwassa kama kiongozi wa chama lakini wanatafakari kuwasilisha malalamiko yao mahakamani.

XS
SM
MD
LG