Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 02:16

Sheria ya Uchaguzi yaleta mabishano Burundi


Wakati sheria juu ya uchaguzi ikiendelea kuzusha migongano ya kisiasa nchini Burundi, wawakilishi wa jamii za kimataifa wameitaka serikali na vyama vya siasa kujadiliana, ili kupata ufumbuzi kuhusu suala hilo. Pia kikao cha bunge kilichokuwa kijadili sheria juu ya uchaguzi utakaofanyika nchini Burundi mwaka 2010 kimeahirishwa kwa muda usiojulikana.

Akihutubia shughuli za kukamilisha kikao cha bunge cha mwezi Juni, spika wa bunge la taifa Pin Havyoanemane, amesema sheria hiyo juu ya uchaguzi itajadiliwa katika kikao cha dharura kitakachofanyika siku zijazo. Alisema kinachotakiwa kufanyika siku za usoni ni majadiliano ya kisiasa kati ya serikali na vyama mbali mbali vya siasa nchini humo, ili mustakbali uweze kupatikana juu ya sheria hiyo.

Wakati huo huo katika mahojiano maalumu na Sauti ya Amerika Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza, anasema hivi sasa kuna amani Burundi na anaelezea matumaini kuwa uchaguzi utakuwa mzuri sana.

XS
SM
MD
LG