Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 05:58

Waasi wa Al-Shabab wataka wanajeshi wa Somalia wasalimishe silaha


Kundi la Al-Shabab limetoa sharti hilo kwa serikali jana jumapili kwa njia ya kanda ya kasseti.Kiongozi wa Al-shabab aliyejitambulisha kama Ahmed Abdi Godane pia anajulikana kama Abu Zubayr alisema majeshi ya serikali yanapewa siku tano kusalimisha silaha zao kwa Al-shabab na kurejea makwao. Anasema viongozi wa serikali watashtakiwa, kwa madai ya kuua raia na kushawishi majeshi ya kigeni kuikalia Somalia.

Godane alikuwa akizungumzia ombi la dharura lililotolewa na serikali mwezi uliopita kwa nchi jirani kupeleka wanajeshi nchini humo kuzuia serikali kuangushwa.

Mkuu wa ulinzi wa serikali, Mohammed Said Yusuf Inda'ade alipuuza tishio hilo akimuelezea Godane kuwa ni mtu ambaye ana khofu ya kuonekana, na hivyo anavaa nguo za kike ili kujificha.

al Shabab na Hisbul Islam wanaishutumu serikali ya kiongozi mwenye msimamo wa kadri, Sharif Sheikh Ahmed kwa kuwa kibaraka wa magharibi na kuapa kumng'oa madarakani.

Wanamgambo wanadhibiti sehemu kubwa ya kusini mwa Somalia, lakini majaribio yao kukamata madaraka Mogadishu yamezuiliwa kutokana na kuwepo kwa walinzi wa amani 4,300 wa Umoja wa Afrika, walinzi hao ni kutoka Uganda na Burundi.

XS
SM
MD
LG