Jimbo hilo limeripotiwa kushuhudia mauaji ya kikabila yanayofanywa na vikosi vya wanamgambo ambavyo vimekuwa vikipigana na vikosi vya serikali kwa miezi 19. Karim Khan aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba uhalifu unafanywa huko Darfur "leo na kila siku" na unatumiwa kama silaha ya kivita.
Alisema uamuzi huo ni matokeo ya "upelelezi wa kina" unaozingatia ushahidi na taarifa zilizokusanywa na ofisi yake.
Sudan ilitumbukia katika mzozo katikati ya mwezi wa Aprili 2023, wakati mvutano wa muda mrefu kati ya wanajeshi wake na viongozi wa kijeshi ulipozuka katika mji mkuu, Khartoum, na kuenea katika mikoa mingine, ikiwa ni pamoja na eneo kubwa la magharibi la Darfur. Miongo miwili iliyopita, Darfur ilishuhudia mauaji ya halaiki na uhalifu wa kivita, uliotekelezwa haswa na wanamgambo wa Janjaweed, dhidi ya watu wanaojitambulisha kama wa asili ya Afrika ya Kati au Mashariki. Hadi watu 300,000 waliuawa na milioni 2.7 walifurushwa kutoka kwa makazi yao.
Forum