Shambulizi la ndege isiyo na rubani kwenye moja ya hospitali za mwisho zinazofanya kazi huko El-Fasher katika jimbo la Darfur nchini Sudan liliuwa watu 30 na kujeruhi kadhaa, chanzo cha watabibu kilisema leo Jumamosi.
Mlipuko wa bomu katika Hospitali ya Saudia Ijumaa jioni ulisababisha uharibifu wa jengo la hospitali hiyo ambako wagonjwa wa dharura walitibiwa, chanzo kiliiambia AFP, kikiomba kutotajwa jina kwa hofu ya kulipiziwa kisasi.
Haijabainika mara moja ni upande upi kati ya hizo zinazopigana za Sudan zilizoanzisha mashambulizi hayo.
Tangu Aprili 2023, jeshi la Sudan limekuwa katika vita na Wanajeshi wa kikosi cha dharura -RSF ambao wameliteka karibu eneo lote la magharibi mwa Darfur.

Forum