Gavana wa Flordia Mrepublican Ron De Santis ametangaza rasmi atagombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2024. Lakini ili kukabiliana na mgombea wa chama cha Demokratic Rais Joe Biden, itamlazimu De Santis amshinde rais wa zamani Donald Trump katika chama cha Republican.
Matangazo ya Duniani Leo kutoka idhaa ya kiswahili ya Sauti Amerika, Washington, D.C.
#habari