Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:05

Marekani: Wanafunzi watatu na watu watatu wauawa katika shambulizi la bunduki shule ya Nashville


Marekani: Wanafunzi watatu na watu watatu wauawa katika shambulizi la bunduki shule ya Nashville
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:20 0:00

Bendera kwenye ikulu ya Marekani pamoja na majengo ya serikali , zitapeperushwa nusu mlingoti hadi machi 31 jioni kufuatia vifo vya wanafunzi watatu na watu wazima watatu kwenye shule ya Nashville katika jimbo la Tennessee, kutokana na shambulizi la risasi Jumatatu, Machi 27.

Katika taarifa yake Rais wa Marekani Joe Biden amesema amechukua hatua hiyo kama heshima kwa walioathiriwa na vitendo visivyokuwa na maana vya vurugu vilivyotokea Jumatatu huko Nashville.
Mshambuliaji mwenye silaha nzito Audrey Hale mwenye umri wa miaka 28 , mwanafunzi wa zamani wa shule ya Covenant , aliyetambuliwa kama mtu aliyebadili jinsia aliuawa wakati akipambana na maafisa wa polisi watano wakati wa shambulizi hilo lililotokea kwenye ghorofa ya pili katika shule ya Presbyterian ambayo inahusiana na kanisa , maafisa wamesema.

XS
SM
MD
LG