Kwa siku ya tatu chama cha Republikan kimeshindwa kumchagua Spika wa kuongoza Baraza la Wawakilishi Marekani. Kiongozi wa chama hicho ameshindwa kupata kura za kutosha. Shinikizo linaendelea. Ijumaa mzunguko wa 12 wa kumchagua spika wa baraza la wawakilishi Marekani umeanza na hakuna mgombea yeyote aliyepata kura 218 zinazohitajika. Wabunge 435 wa Marekani wameanza mzunguko wa 12 kumchagua spika wa baraza la wawakilishi ambapo hakuna matumaini kwa Kevin McCarthy kupata ushindi licha ya kufanikiwa kuongeza kura chache kutoka kwa wapinzani wake. Endelea kusikiliza historia ya uchaguzi wa Spika wa Marekani na yale ambayo yanatarajiwa kutokea kutoka kwa mchambuzi wetu. Endelea kusikiliza...
Matukio
-
Machi 14, 2025Changamoto za ulezi wa watoto walemavu kiakili Kenya
-
Februari 28, 2025Waislamu wajitayarish kwa Ramadhani
-
Februari 27, 2025Ethiopia na Somalia waimarisha uhusiano wao
-
Februari 18, 2025Nini kilichosababisha Raila Odinga kushindwa katika uchaguzi wa AU?
-
Februari 11, 2025Naibu Katibu Mkuu aeleza hatua za dharura zinazochukuliwa DRC