Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 02, 2024 Local time: 04:10

DRC imemuita balozi wake wa Kigali, Kagame amezungumza na katibu mkuu wa umoja wa mataifa


Waandamanaji wakiwa kwenye mpaka wa DRC na Rwanda wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe unaodai kwamba Rwanda na Uganda wanaunga makundi ya waasi nchini DRC. Oct 31, 2022
Waandamanaji wakiwa kwenye mpaka wa DRC na Rwanda wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe unaodai kwamba Rwanda na Uganda wanaunga makundi ya waasi nchini DRC. Oct 31, 2022

Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imemuita balozi wake wa Rwanda kurudi Kinshasa kwa mashauriano.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya DRC inasema “Kinshasa inatoa maelekezo kwa balozi balozi wake mpya nchini Rwanda, kuahirisha majukumu yake nchini Rwanda.”

Uamuzi huo umetolewa saa chache baada ya DRC kumfukuza balozi wa Rwanda mjini Kinshasa.

Rwanda na DRC zimeimarisha usalama wake huku kukiwepo shutuma za Rwanda kuunga mkono kundi la waasi la M23 mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi ametuma Meja Jenerali Bruno Mpezo Mbele, kamanda mkuu wa kikosi maalum katika Kivu kaskazini, kuongoza oparesheni dhidi ya waasi wa M23.

Maandamano ya raia wa DRC

Mamia ya raia wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wameandamana hadi mpakani mwa Rwanda na DRC, n ahata kuchoma bendera za Rwanda, wakidai kwamba Rwanda inaunga mkono kundi la waasi la M23.

Rwanda imekuwa ikikana kila mara madai hayo. Rwanda inadai kwamba DRC inaunga mkono waasi wa FDLR wenye nia ya kutatiza usalama nchini Rwanda, madai ambao DRC vile vile imekanusha.

Mapigano makali yanaendelea kati ya kundi la waasi la M23 na wanajeshi wa serikali ya DRC.

Mazungumzo kati ya Kagame na Mkuu wa UN

Rais wa Rwanda Paul Kagame ameandika ujumbe wa twiter kwamba amefanya mazungumzo na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres kuhusu uhasama unaoendelea kati ya Rwanda na DRC.

“saa chache zilizopita, zimezungumza na katibu mkuu wa umoja wa mataifa kuhusu hali nchini DRC,” ameandika Kagame katika ukurasa wake wa twiter, akiongezea kwamba njia ya kupunguza uhasama na kusuluhisha maswala yenye utata ni kutekeleza makubaliano ya Nairobi na Luanda, pamoja na juhudi zingine za kimataifa. Tunastahili kutekeleza makubaliano hayo.”

XS
SM
MD
LG