Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 21:11

Senegal: Asasi za kiraia zamtaka Macky Sall kutangaza kama atawania tena urais


Rais wa Senegal Macky Sall (Reuters)
Rais wa Senegal Macky Sall (Reuters)

Mashirika kadhaa nchini Senegal, yanamtaka Rais Macky Sall kuondoa shaka, na kutangaza hadharani kwamba hatagombea muhula wa tatu, jambo ambalo walisema linaweza kuzua "machafuko."

Sall, ambaye alichaguliwa mnamo mwaka wa 2012 na tena mwaka wa 2019, kwa miezi kadhaa sasa haijafahamika ikiwa anakusudia kugombea muhula wa tatu mwaka wa 2024.

Katiba ya nchi hiyo haimruhusu rais kuhudumu kwa zaidi ya mihula miwili mfululizo. Lakini wafuasi wa Rais Sall, wanasema kuwa marekebisho ya katiba ya mwaka 2016 yalibadilisha sheria hiyo.

Upinzani unaahidi hatua kali ikiwa Sall, ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, atawania muhula mwingine.

Katika taarifa Alhamisi, mashirika ya haki za binadamu na demokrasia yalitaja matokeo "ya kusikitisha hasa" ya majaribio ya kulazimisha mihula ya tatu kwingineko barani Afrika.

Suala hilo ambalo nchini Guinea na Ivory Coast limesababisha ghasia za machafuko. Mashirika yasiyo ya kiserikali yalisema yalitaka "kuepuka hali ya machafuko" katika nchi inayojulikana kwa utulivu wa kisiasa ikilinganishwa na eneo lote.

XS
SM
MD
LG