Sall ameagiza wizara ya haki kuthathmini haraka iwezekanavyo, uwezekano wa kuwepo mpango wa kutoa msamaha kwa watu waliopoteza haki ya kupiga kura.
Lengo la hatua ya Sall ni kupunguza uhasama wa kisiasa ambao umekuwa ukiongezeka katika miezi ya hivi karibuni.
Joto la siasa limeongezeka Senegal kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Wanasiasa maarufu wa upinzani akiwemo aliyekuwa meya wa Dakar Khalifa Sall na Karim Wade ambaye ni mwanae aliyekuwa rais wa nchi hiyo Abdoulaye Wade, waliofunguliwa mashtaka ya ufisadi.
Khalida alihukumiwa mwaka 2018. Wade alihukumiwa mwaka 2015.
Waliachiliwa huru lakini hawakuruhusiwa kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2019 ambao rais Sall alishinda. Wanadai kwamba mashtaka dhidi yao yalichochewa kisiasa.