Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 19:17

Mazungumzo ya mzozo wa Ethiopia yaingia siku ya pili


Kifaru cha kijeshi nchini Ethiopia.
Kifaru cha kijeshi nchini Ethiopia.

Mazungumzo rasmi ya kwanza ya amani kati ya pande zinazozozana katika vita vya kikatili vya miaka miwili katika eneo la Tigray nchini Ethiopia yaliingia siku ya pili Jumatano nchini Afrika Kusini.

Yakiongozwa na Umoja wa Afrika (AU), mazungumzo hayo mjini Pretoria yanafuatia kuongezeka kwa mapigano makali katika wiki za hivi karibuni, ambayo yameitia wasiwasi jumuiya ya kimataifa na kuzua hofu kwa raia waliojipatya katika mapigano hayo.

Mazungumzo hayo yanafanyika katika makao makuu ya wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini.

Mjumbe wa AU Pembe ya Afrika na rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, ambaye ni msimamizi mkuu wa mazungumzo hayo, alipigwa picha na waandishi wa habari wa AFP wakiingia ukumbini Jumatano asubuhi.

Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta ,ambaye ni sehemu ya timu ya upatanishi, pia alionekana akiingia ndani ya jengo hilo, sawa na makamu wa rais wa zamani wa Afrika Kusini Phumzile Mlambo-Ngcuka.

XS
SM
MD
LG