Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 28, 2023 Local time: 22:16

Ramaphosa aeleza matumaini ya tija katika mazungumzo ya amani kati ya Ethiopia na TPLF


Mzozo wa Ethiopia Eritrea na Tigray
Mzozo wa Ethiopia Eritrea na Tigray

Rais wa Afrika Kusini amesema ana matumaini ya tija katika mazungumzo ya kwanza rasmi ya amani yenye lengo la kumaliza vita vya miaka miwili, kati ya jeshi la Ethiopia na vikosi vya eneo la kaskazini mwa nchi hiyo la Tigray, yaliyoanza nchini Afrika Kusini Jumanne.

Mazungumzo hayo yananuiwa kumaliza mgogoro ambao umepelekea vifo vya maelfu ya watu, mamilioni kuyahama makazi yao na kuwaacha maelfu katika hali mbaya ya njaa katika taifa hilo la pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika, hali inayoelezwa kuyumbisha eneo zima la Pembe ya Afrika.

Mazungumzo hayo yatakamilika Jumapili, serikali ya Afrika Kusini ilisema.

Afrika Kusini "inatumai mazungumzo yataendelea kwa njia yenye tija na kuleta mafanikio ambayo yatasababisha amani ya kudumu kwa watu wote wa nchi dada yetu mpendwa Ethiopia," alisema Vincent Magwenya, msemaji wa Rais Cyril Ramaphosa.

Timu ya upatanishi ya Umoja wa Afrika inaongozwa na Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, akisaidiwa na rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu rais wa zamani wa Afrika Kusini, Phumzile Mlambo-Ngcuka.

Umoja wa Mataifa na wawakilishi wa Marekani walishiriki kama waangalizi, Umoja wa Afrika ulisema.

Mazungumzo hayo, yanayoongozwa na Umoja wa Afrika, yanaanza wakati serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed imedai kupata mafanikio makubwa katika vita hivyo na kuiteka miji kadhaa mikubwa ya Tigray katika wiki iliyopita.

Mashambulizi hayo ya serikali yaliyofanywa kwa pamoja na wanajeshi washirika kutoka nchi jirani ya Eritrea, yameibua hofu ya madhara zaidi kwa raia, na kusababisha viongozi wa Afrika, Marekani na Ulaya na hata Papa Francis kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano na mazungumzo ya haraka.

XS
SM
MD
LG