Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 10:22

Tutasimama kidete na Ukraine, viongozi wa G7 wamhakikishia Zelensky


Bendera za nchi wanachama wa G7
Bendera za nchi wanachama wa G7

Viongozi wa kundi la mataifa Saba tajiri zaidi duniani, G7, waliokutana Jumanne kwa njia ya video na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, waliahidi kwamba "watasimama kidete na Ukraine kwa wakati wote" baada ya Russia kuendeleza mashambulizi yake ya makombora katika miji ya Ukraine.

Walisema katika taarifa baada ya mkutano huo kwamba wamemhakikishia Zelenskyy hawajakatishwa tamaa, na kwamba wako imara katika "dhamira yetu ya kutoa msaada unaohitajika na Ukraine, ili kudumisha uhuru wake na uadilifu wa kieneo."

Walisema "mashambulizi ya kiholela ya Moscow dhidi ya raia wasio na hatia ni uhalifu wa kivita."

"Tutawajibisha Rais Vladimir Putin na wale wanaohusika," viongozi wa G-7 walisema.

G-7 inajumuisha Marekani, Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Italia, Kanada na Japan. Huku kukiwa na vitisho vinavyoendelea vya Putin kutumia silaha za nyuklia, G-7 ilikariri kuwa kutakuwa na adhabu kali iwapo Moscow iwapo itatumia silaha za maangamizi makubwa, lakini haimaanishi kuhusika moja kwa moja kijeshi nchini Ukraine.

Maafisa wa Marekani wamesema hawajaona dalili kwamba Putin ameamua kutumia silaha za nyuklia na kusisitiza kuwa hakuna mabadiliko katika msimamo wa Marekani kuhusu nyuklia.

XS
SM
MD
LG