Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 21:01

Kimbunga Ian nchini Marekani kinatabiriwa kuingia Virginia


Kimbunga Ian katika jimbo la South Carolina na kinatabiriwa kuingia jimbo la Virginia na West Virginia
Kimbunga Ian katika jimbo la South Carolina na kinatabiriwa kuingia jimbo la Virginia na West Virginia

Majimbo ya Florida, North na South Carolina yanakabiliwa na changamoto kubwa leo Jumamosi kutokana na uharibifu uliofanywa na kimbunga Ian, baada ya moja ya dhoruba kali zaidi kuwahi kushambulia Marekani na kusababisha uharibifu wa mabilioni ya dola pamoja na kuua zaidi ya watu 20.

Picha mpya kutoka kwa idara ya taifa inayohusika na masuala ya Bahari na Anga zilionyesha nyumba kadhaa za pwani na jengo la mahoteli lililokuwa kwenye mwambao wa Kisiwa cha Sanibel cha Florida zilichukuliwa na maji kutokana na kuongezeka kwa dhoruba Ian. Ingawa nyumba nyingi zilikuwa bado zimesimama, zilionekana kuwa na uharibifu wa paa, picha hizo zilionyesha.

Kimbunga Ian, ambacho sasa ni kimbunga baada ya kitropiki, kilikuwa kinadhoofika lakini bado kinatabiriwa kuleta hali mbaya Jumamosi katika sehemu za majimbo ya North na South Carolina, Virginia na West Virginia, kulingana na kituo cha Kitaifa kinachofuatilia Kimbunga.

XS
SM
MD
LG