Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 16:25

Kimbunga Ian chaharibu takriban nyumba 80,000 katika mji wa Fort Mayers


Muonekano wa angani wa boti na mali zilizoharibika baada ya Kimbunga Ian kusababisha uharibifu mkubwa huko Fort Myers, Florida, U.S., Septemba 30, 2022. REUTERS/Shannon Stapleton.
Muonekano wa angani wa boti na mali zilizoharibika baada ya Kimbunga Ian kusababisha uharibifu mkubwa huko Fort Myers, Florida, U.S., Septemba 30, 2022. REUTERS/Shannon Stapleton.

Waakazi wa Florida wenye huzuni wameanza kurejea katika makazi yao kutoka maeneo waliyokuwa wamehama kutokana na kimbunga Ian na kutathmini uharibifu uliozuka tangu jumatano.

Kimbunga Ian kimeharibu takriban nyumba 80,000 katika mji wa Fort Mayers, katika kile wakuu wa jimbo wanasema ni uharibifu mkubwa kuwahi kushuhudiwa. Nyumba za kuhamishika nazo zimeharibiwa wakati barabara na madaraja vimebomolewa.

Hakuna umeme , hakuna maji safi na hata boti za gharama kubwa zimeharibiwa , hiki ni kimbunga kibaya kuwahi kutokea. Chini ya saa 24 baada ya maji kupungua , wakaazi waliohamishwa walikuwa wanarejea Fort Mayers pole pole ili kuona ikiwa nyumba zao zimenusurika na dhoruba hiyo kubwa.

Kimbunga Ian kilichoibuka tena kimeonekana Ijumaa kuelekea North Carolina siku moja baada ya kuondokana kutoka pwani ya mashariki ya Florida.

Juhudi za uwokozi zinaendelea na maafisa wanasema karibu watu 800 waliokwama ndani ya nyumba zao wameokolewa hadi hii leo na karibu 12 wamefariki kutokana na kimbunga hicho cha hatari.

Kituo cha taifa cha udhibiti wa vimbunga marekani, NHC kimesema Kimbunga Ian kilichopungua nguvu kufikia kiwango cha chini cha namba moja kinaelekea south Carolina leo Ijuma kutokea bahari ya atlantic ,.

XS
SM
MD
LG