Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:36

Cameroon yaadhimisha Siku ya Shirika la Msalaba Mwekundu Duniani


Bendera ya Shirika la Msalaba Mwekundu.
Bendera ya Shirika la Msalaba Mwekundu.

Siku ya msalaba mwekundu imeadhimishwa nchini Cameroon Jumapili, huku mamia ya wafanyakazi kutoka shirika hilo kwenye miji na vijiji kote wakiomba kutambulika na kulindwa na jumuiya zao.

Watendaji wa masuala ya kibinadamu wanasema ingawa hawajaripoti vifo, wafanyakazi hao wa msalaba mwekundu ni waathiriwa wa mashambulizi mabaya yanayofanywa na kundi la Boko Haram na ghasia za wale wanaotaka kujitenga.

Mamia ya watu wakiwemo wanufaika wa shirika hilo, wafanyakazi wa masuala ya kibinadamu na maafisa wa serikali walikusanyika katika makao makuu ya shirika la Msalaba Mwekundu huko Younde kusherehekea siku hii inayoadhimishwa leo Marchi 8.

Miongoni mwao ni Aiou Alim mfanyakazi wa kujitolea wa shirika hilo aliyefanyakazi katika mji wa kaskazini wa Banyo, kwenye mpaka wa Cameroon na Nigeria.

Anasema mwezi machi yeye na wafanyakazi wenzake saba walishikiliwa mateka na watu waliokuwa wanawashauri kuchukua chanjo ya COVID 19 huko Banyo.

Anasema waliachiliwa baada ya maafisa wa ndani wa serikali kutoa maelezo kwa watekaji kuwa shirika la msaba mwekundu liko nje ka wa ajili ya kuokoa maisha ya watu.

Anasema kila raia wa Cameroon anastahili kupewa taarifa kwamba shirika la msaba mwekundu kazi yake ni kuokoa maisha ya watu.

XS
SM
MD
LG