Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 14:00

Kikosi cha pamoja cha kijeshi kimeua zaidi ya waasi 100 eneo la ziwa Chad


Ramani ya ziwa Chad na maeneo jirani
Ramani ya ziwa Chad na maeneo jirani

Kikosi cha pamoja cha kijeshi kutoka Nigeria, Niger na Cameroon kilisema Jumapili kwamba kimewaua zaidi ya waasi 100 wa kiislam wakiwemo makamanda 10 katika wiki chache zilizopita huku wakizidisha mashambulizi ya ardhini na angani katika eneo la ziwa Chad.

Wapiganaji wa Boko Haram na kundi lililojitenga la Islamic State West Africa Providence (ISWAP) kwa zaidi ya muongo mmoja wamekuwa wakipambana na jeshi la Nigeria katika mzozo ambao umeyatumbukiza mataifa jirani.

Msemaji wa kikosi kazi cha pamoja cha kimataifa kanali Muhammad Dole alisema wanajeshi wamejitosa katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi katika eneo la Ziwa Chad na kupata silaha kadhaa, vyakula na dawa haramu.

Katika kipindi cha operesheni hii zaidi ya magaidi 100 wameondolewa wakiwemo zaidi ya makamanda kumi wa vyeo vya juu kufuatia mashambulizi ya anga yaliyoendeshwa kijasusi katika visiwa vya ziwa Chad na vikosi vya anga Dole alisema.

XS
SM
MD
LG