Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:01

WHO yasema bado kiwango cha utoaji chanjo kiko chini barani Afrika


Dkt. Matshidiso Moeti, Mkurugenzi  wa WHO wa kanda  ya Afrika (Photo courtesy of WHO)
Dkt. Matshidiso Moeti, Mkurugenzi  wa WHO wa kanda  ya Afrika (Photo courtesy of WHO)

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema kiwango cha chanjo katika bara la Afrika bado kiko chini sana, wakati bara hilo likipambana kufikia asilimia 70 ya watu waliopokea chanjo.

Mkurugenzi wa WHO wa kanda ya Afrika, Matshidiso Moeti amesema mwaka mmoja tangu program ya COVAX ilipopeleka chanjo za kwanza za COVID-19 katika bara la Afrika, karibu dozi milioni 400 zimetolewa ikiwa ni zoezi kubwa la chanjo kufanyika kwa mwaka mmoja.

Ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao , mjini Brazaville, Jamhuri ya Congo.

Hata hivyo kiwango cha chanjo katika bara hilo ni kidogo duniani, ikiwa ni asilimia 13 ya waafrika waliochoma chanjo kamili.

Nchi 18 zimetoa chanjo chini ya asilimia 10 ya watu wake na nchi tatu zimechanja watu wake chini ya asilimia moja.

Nchi 29 zimetumia chini ya asilimia 50 ya chanjo zake , kwa mujibu wa taarifa .

Phionah Atuhebwe afisa wa chanjo WHO Africa, amesema haya:"kwa bahati mbaya watu walio katika hatari zaidi barani Afrika bado hawajachanjwa. Katika nchi 27 ambazo zinaripoti Data juu ya chanjo kwa mfanyakazi wa afya, theluthi moja tu ya watu wamechanjwa.

Miongoni mwa nchi 24 ambazo zinatoa Data za chanjo kwa wazee, ni asilimia 21 tu ya watu wazima wenye umri wa zaidi ya miaka 50 waliopatiwa chanjo kamili. Ni asilimia 11 tu ya watu wenye magonjwa mbalimbali wanaripotiwa kupewa chanjo kamili katika nchi 20 ambazo zinatupatia Data hizi.”

Lakini Afrika inapambana kufikia lengo kwa kushirikiana na wadau wengine, amesema atuhebwe. WHO itafanya uhamasishaji mkubwa wa shughuli za chanjo ya COVID-19 kwa awamu tofauti mwaka huu.

Itatoa msaada kwa nchi 20, ambapo 10 tayari zimeanza kampeni za chanjo kwenye maduka makubwa, masoko na vijiji vya mbali, amesema afisa.

Kwa kila kitu ambacho kimewekwa Afrika inatakiwa kufikia asilimia 70 ya watu waliochanjwa ifikapo mapema mwaka 2023.

XS
SM
MD
LG